NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 3 - TRUST ME

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, April 15, 2018

NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 3

TULIPO ISHIA........ 
Jamani mbona ghafla hivi hata hamsemi, Peter na Pricila walitazamana kisha wakatabasamu, kisha mama akasema tena mmmh mwanangu mpaka tumbo linakua hivi hata usemi nije kukusaidia kazi nyumbani jamani tunaugomvi?
                                 

SASA ENDELEA.......
kamaana desturi za waafrika mama mwenye mimba anahitaji ukaribu sana aswa wa wazazi au uongo mume wangu?mama Peter alisema huku akimtazama mumewe kama hakukua na tatizo lolote, mume akajibu kabisa mke wangu mimi pia nimewaeleza hili.

 Peter aliomba msamaha kwa kitendo hicho alikiri kwamba hatorudia tena, baba alitania tena, kwahiyo unampngo wa kuweka tena basi walicheka sana. Baadae mama Peter alimchukua Pricila na kwenda jikoni,

 waliandaa chakula huku Peter na baba yake waliendelea kupiga hadithi na wakifurahi pamoja.
 Chakula hakikuchelewa sana baada ya muda walianza kuandaa jamvini, na kuwakarisha wanaume kula chakula kile, chakula kilisifiwa sana, baba Peter alikua mtu wa utani sana akasema "

mke wangu leo chakula kitamu au kwakua kunawageni kisha alicheka, mama Peter akajibu baba Peter na utani jamani ujue tumezeeka sasa ujukuu ndiyo huo, wote walicheka tena.
kwakua wote walikua wamechoka na uchovu, Peter aliomba wakalale nakuhaidi wataongea vizuri siku itakayofuata, basi mama aliinuka nakuwaelekeza chumba kilichoandaliwa kwa ajili yao.

Peter na mke wake waliaga wazazi wao nakuelekea chumbani walipoelekezwa, walipofika chumbani Pricila alisema"mume wangu yaani nmefurahi sana wazazi wametupokea vizuri mpaka sio vizuri"


alitabasamu kisha akasema nakupenda mume wangu, Peter alitamkumbatia mkewe kisha akasema nakupenda zaidi mke wangu kwetu ni kwako pia kua na amani kisha alimbusu mkewe. Walijiandaa kwaajili ya kulala kisha wakapanda kitandani,

Pricila akaweka kichwa kifuani kwa mumewe na baadae akapitiwa na usingizi Peter alipojiridhisha mkewe kalala nae akalala. Mama peter aliingiza vyombo ndani kisha akaingia chumbani kulala mume nae alifuata,

alipofika chumbani alikuta mkewe tayari yu kitandani kajilaza kisha baba Peter akasema naona leo umefurahi sana kumuona mwanao, mama Peter akajibu sanaaaa, baba Peter aliendelea lakini mke wangu kilichotokea mchana wa leo ni kweli au ulikua unatania,

kisha alijichekesha, mama Peter kwa hasira pale kitandani hivi wewe mwanaume unanitakia nini?unanitakia nini nakuuliza mbona kunifuatilia sana ee?aliongea kwa ukali, nisamehe mke wangu baba Peter aliongea kwa upole, mama Peter alisonya kisha alijifunika gubigubi,

baba Peter alimtizama mke wake akatikisa kichwa pia alilala, lakini akiwa amejilaza akili ilimjia yakutolala mazima hivyo akaigiza kalala. Mama Peter taratibu alifunua shuka akamchungulia mumewe akamtikisa, baba Peter alijikausha kimya,

mama Peter alipojiridhisha mumuwe kalala, alishuka kitandani kwa tahadhari, alipofika chini alivua nguo zake kisha akainamana uvunguni akavuta kaniki lake jeusi,

 akajichora mwili mzima kisha akachua usinga wake mweusi akapiga pale kitandani alipokua kalala akatokea mtu kama yeye,

 baba Peter aliogopa sana kwani alikua akishuhudia yote hayo lakini alijikaza kiume, daaaaa ningekua mimi hapo ningetoka nduki kwakweli angeniua tu sijui wewe ungefanya nini?

 mama Peter alipoyeyuka baba Peter alipagawa sio kidogo. Aliketi chini kwani aliogopa mfano wa mtu aliyelala nae kitandani ilihali kaona mkewe akipotea, basi alishuka chini akaketi akilia sanaa.

Mama Peter alifika porini, lakini palikua pamechangamka watu wengi waume kwa wake, wakicheza ngoma kwa furaha kama si usiku.

Basi mama Peter alifurahi sana kuona watu wakiwa na furaha basi alipiga makofi ghafla kukawa kimya, kisha akasema nina furaha sana ila kama nilivyosema kikao kilichopita kwamba nimechoka sana majukumu yamekua mengi hivyo nilikua nikitafuta mrithi wangu lakini habari njema ni kwamba mkwe wangu ni mjamzito hahhahaha, alicheka,

kisha watu wote walicheka na ngoma ikapigwa walicheza kidogo kisha ngoma ikazimwa akaendelea, lakini siku hizi sina furaha hata kidogo mume wangu anajua kila kitu kuhusu mimi hivyo ananifuatilia sana,

sasa ndugu zangu sijui nimfanye nini?wote walikaa kimya kisha akasema "nawapa muda tukirudi hapa mje na majibu watu wote pale walionyesha sura za hudhuni, mama Peter aliwaamuru waondoke na wote walipotea na yeye alikua wa mwisho kufanya hivyo,

alipoyeyuka alifika katika kona ileile na kumbuka baba Peter hakulala alikua akilia tu. Basi alipofika pale ile anageuka tu waligongana macho, mama Peter aliishiwa nguvu kwa aibu aliyokua nayo alipiga magoti chini asijue la kufanya. Baba Peter alimsogelea mkewe

nakusema"ASANTE MKE WANGU SIKUJUA NAISHI NA NYOKA"Kisha aliinuka macho yakiwa yamevimba kwakulia,
  mama Peter alitama dunia ipasuke ajifiche lakini haikuwezekana basi alivua nguo zake nakutoka nje kuomba msamaha, alifika nakuanza kulia akisema nisamehe mume wangu najua nmekuumiza nakuhaidi sitorudia tena,

 baba Peter alimtizama mkewe kwa huruma kisha akasema mke wangu mungu akusamehe kwakua hujui hufanyalo maana hukumu yako ni kubwa kisha alimuomba aingie ndani maana kulikua kunaelekea kukucha.

Nakweli asubuhi ilikua imefika Peter na mkewe waliamka walishangaa tayari wazazi wameamka baba anafagia na mama anaosha vyombo.

ITAENDELEA............. SEHEM YA 4
Imeandikwa na kutungwa
                                       A AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter 

USISAHAU KUCOMMENT APO CHINI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here