NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 8 - TRUST ME

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, April 24, 2018

NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 8

TULIPO ISHIA.............
Ayubu roho ilimuuma machozi yalimdondoka tu alipoangalia pembeni aliona chakula lakini hakijaguswa alipojaribu mlisha baba Peter pia alishindwa na kutapika

SASA ENDELEA.........

 tena, na alikua anatapika maji tu kwani hakula chochote tena maji yenye harufu kali, baba Peter alionesha ishara ya mikono akimshukuru na pia alimruhusu aondoke asijekutwa na mkewe ikawa balaa. Ayubu alielewa hilo ila aliondoka kwakusikitika sana,

alipoondoka tu mama Peter alikua kafika tayari, je mzee Ayubu atafanya nini kwaajili ya rafiki yake, mama Peter naye atajulikana au mmh, Mama Peter alitambua hilo lakini hakutaka kujishugulisha nalo kwani yeye hakujali mtu

yeyote alijiamini na alichokifanya, alimsogelea mume wake na kusema "kwahiyo umegoma kula, mimi nimepika wewe hujala, hujui nilipika kwaajili yako,

sasa siku nyingine utajipikia", baba Peter hakua na neno zaidi yakumuangalia mke wake na kufuta jasho lilokua likimwagika usoni kwakutumia shati alilokua amevaa.

Mzee Ayoub alifika nyumbani akiwa amepoa sana kwani hali aliyoiona kwa rafiki yake ilimsikitisha sana. "mume wangu, mbona haupo sawa?,

kuna nini huko hutokako,?, alikua ni mke wa mzee Ayoub akimuuliza mume wake kuhusu nyumbani kwa baba Peter., mzee Ayoub alimuangalia mkewe kisha akasema, "

mke wangu yale tuliyokua tukiyasikia ni sahihi maana kwa hali yakawida haiwezekani, alipofika hapo alishusha pumzi mmmmh!!!!, nmemkuta baba Peter hoi, anatapika,

anahrisha na anavuja jasho si kawaida lakini mkewe hayupo na kamuachia chakula tu bila kujali mwenzie hatoweza kula, baba Peter analia tu na chakushangaza alinionesha ishara niondoke nafikiri alihofia mkewe kunikuta pale, lazima kutakua na kitu,

mzee Ayoub alimaliza kwa masikitiko sana, mkewe alikua akitikisa tu kichwa alipokua akimsikiliza mumewe, "tutafanya nini sasa mume wangu tumsaidie maana ile ni familia ya mtu, tusijeonekana tuna viherehere",

mama Ayoub aliongea kisha mumewe alisema nina hakika Peter hatambui hili kwakua nina mawasiliano yake ni lazima kesho asubuhi nitaenda mjini nikampe taarifa ila hili linabidi liwe siri kati ya mimi na wewe kwani akijua yule mwanamke hatotuelewa hata kidogo, sawa mume wangu, mkewe alimalizia, 

walikubaliana asubuhi Mzee Ayoub aende mjini kwa Peter.  muda tayari ulikua umekwenda sana, mzee Ayoub na mkewe walifanya maandalizi kwa ajili ya safari ya kesho na mama alimsisitiza mume wake kua makini sana.

Mume alimuelewa sana mke wake na kusema usijali mke wangu. Basi asubuhi ilifika na mzee Ayoub alianza kujiandaa kuondoka aliagana na mke wake na kuanza safari ya kwenda mjini.

Basi mzee Ayoub alinunua muda wa maongezi nakumpigia Peter, Peter alipokea simu ile na mazungumzo yakawa hivi, Peter:haloo baba, shikamoo Mzee Ayoub:marahaba

mwanangu mimi nipo mjini hapa nina shida na wewe hivyo basi naomba unifuate, Peter:sehemu gani Baba yangu, mzee Ayoub alimuelekeza Peter alipo kisha Peter

akasema"samahani baba yangu kwasasa nashindwa kutoka kazini ila nampigia simu mke wangu akufuate hapo sasa hivi, mimi nitakukuta nyumbani,

sawa mwanangu, mzee Ayoub alikubali. Basi baada ya simu kukatwa Peter alimpigia simu mke wake, baada ya muda Pricila alikwisha jiandaa, alichukua pikipiki nakumfuata mzee Ayoub,

mzee Ayoub alifurahi kumuona Pricila basi walisalimia kisha Pricila aliagiza pikipiki nyingine kwaajili ya mzee Ayoub nakurudi nyumbani.

Walipofika nyumbani Pricila alimkaribisha baba Yule vizuri na kwa nidhamu alimpatia juice, na kisha alimuacha mzee Ayoub sebuleni akitizama runinga na yeye kuandaa chakula kwani jioni ndiyo ilikua inaingia kwa muda ule.

Pricila alipokua jikoni, mumewe aliingia nayeye pia alifurahi sana kumuona mzee omba mzee Ayoub akaoge ili ajisikie vizuri kisha arudi kwa ajili ya chakula pia alimchukua mumewe pia akaoge kwani alichoka na kazi.

 mzee Ayoub alioneshwa chumba chake, alioga kisha alirudi sebuleni, Peter pia alimaliza kuoga alirudi sebuleni.

Pricila aliandaa chakula na baada ya hapo walikula walimaliza, ndipo Pricila alimchukua mwanae kwa yule dada wa kazi na kuaga kwamba anakwenda kumyonyesha mwanaye kwani alihisi mzee Ayoub lazima anajambo hivyo aliwapa Uhuru.

Pricila alipoondoka mzee Ayoub alisogea alipokua ameketi Peter akasema"mwanangu kuna kitu nataka kukueleza ila yataka ujasiri sana, "

Peter alihoji kuna nini tena?ndipo mzee Ayoub aliposema kila kitu kilichotokea nyumbani, tena aliongea kwa uchungu, Peter alilia sana kisha akasema najua huyo ni mama anataka muua baba yangu,

NAMCHUKIA SANA MAMA YANGU, kwanini katili hivi, mzee Ayoub akauliza kwanini unahisi ni mama yako?
 
 Peter hakuona sababu ya kumficha chochote mzee Ayoub, alimwambia yote aliyoambiwa na baba yake kuhusu mama yake, mzee Ayoub hakutaka kuhoji sana kwani alihofia kuzidisha machozi kwa Peter,

alimtia moyo kwakusema"mwanangu Peter kwasasa huna sababu yakufanya hayo yote maana baba anaumwa nenda kapumzike kesho jiandae na safari",

Peter aliinuka na kumuaga mzee Ayoub kwa hudhuni sana, mzee Ayoub hakusema kitu zaidi alitikisa kichwa kwa ishara ya kuonesha anamhmuhurumia Peter.

Basi safari hii Peter alishindwa kujizuia kabisa kwani alipofika chumbani alikua bado analia,

mkewe hakua amelala hivyo aliinuka kitandani na kumsogelea mume wake nakusema, "

mume wangu kuna nini?Peter alishindwa jibu zaidi aliita mama, "mama, mama utamuua baba yangu, "kauli hiyo ilimuogopesha sana Pricila kisha akauliza tena,

mbona sikuelewi atamuua vipi sasa", niweke wazi na mimi nikuelewe basi, Peter hakuficha hata kidogo alijikuta akimueleza mkewe kila kitu, Pricila alilia sana,

kwanza aliwapenda wazazi hao pili alimuonea huruma baba yake kisha tatu aliogopa sana wachawi kisha akasema"Peter namuogopa mama mimi jamani,

namuogopa, Peter alijua pale ameharibu kumpa Pricila habari zile kwani atakua na kazi yakumbembeleza aelewe na kumhaidi kesho atakwenda shughulikia"

mke wangu usilie niombee mumeo kesho nikienda nikafanikishe jambo hili kwani lahitaji Mungu bila hivyo hata mimi nitapotea, kwahiyo niombee mumeo",

usiku huo wawili hao hawakulala kabisa wakisuburi kesho. Kesho asubuhi waliamka, Pricila alimuandaa mumewe na kisha walikunywa chai pamoja na mzee Ayoub,

safari ilianza. Ilichua muda kiasi mpaka kufika katika kijiji chao na walipokua njiani ukimya ulitawala.

Waliingia kijijini mishale ya mchana mchana lakini kabla hawajafika nyumbani mzee Ayoub aliombwa kushushwa njiani,

Peter Mimi niache tu hapa siunajua mama yako hakijua kama mimi nilikuja kukupa taarifa hapatakalika, mzee Ayoub alimwambia Peter,

ni kweli baba basi shuka hapa ila jitahidi sana leoleo ufike nyumbani ili nipate muda wakuzungumza na wewe, Peter alimuomba mzee Ayoub.

Basi mzee Ayoub na Peter walifanya makubaliano hayo na hatimae Peter aliendelea na safari, alifika nyumbani alimkuta mama yake akiwa anasuka mkeka wake, mama alipomuona Peter alishtuka sana, alijiuliza maswali moyoni bila kupata majibu, mmmmh sijui kafuata nini?, mimi

sikupenda amuone baba yake mapema yote hii, mama Peter alijisemesha moyoni. Basi aliinuka na kusema,

mwanangu Peter karibu jamani, karibu sana, lakini mbona "ghafla hivi?, kwema kweli?, au nyumbani kuna matatizo?alijikuta akauliza maswali mfululizo,

Peter akasema "mama mbona maswali mengi jamani kwani tatizo mimi kuja kwetu?nae aliuliza, tehtehteh!!!mama alijichekesha nakusema hakuana shida karibu mwanangu.

 Peter alipokua anaketi katika mkeka uliotandikwa pale chini alishuhudia kuona baba yake anatoka ndani kwa magoti kwani mwili wake haukua na nguvu hata kidogo, Peter aliita babaaa,

huku akimkimkimbilia baba yake, alimtizama baba yake usoni nakuanza kulia hakutaka kuhoji sana kwani mzee Ayoub alimsimulia kila kitu.

Alimgeukia mama yake nakusema"mama mpaka baba anaumwa hivi husemi, nini lengo lako mama yangu?, je unataka baba afe ndiyo furaha yako?,

mama hakua najibu zaidi yakujikuna kichwani. Baba Peter alidhoofika sana, basi Peter alijikokota na baba yake mpaka kwenye ule mkeka, mama kama kuna chakula naomba, Peter aliomba, mama aliiinuka nakumpatia kisha Peter alijaribu kumpa baba yake lakini baba alitapika.

Peter alipokua akihangaika na baba yake, mzee Ayoub na mkewe walifika,

walikaribishwa vizuri sana, mama Ayoub alimuhurumia baba Peter kwani alikua na hali mbaya sana. Walipomaliza maongezi walimuaga mama Peter na baba Peter na kuhaidi kurudi kesho yake lakini Peter aliwasindikiza wageni wale kwani alikua na mazungumzo nao. "

Mzee Ayoub na mama kama mnavyomuona baba yangu na ninyi ndiyo familia yangu, naombeni msaada nafanyaje hapa"Peter aliwaambia wazee wake, mzee Ayoub akasema kuna mtaalamu kijiji jirani naimani atatusaidia kama upo tayari kesho mapema twende,

mama Ayoub pia alitikisa kichwa kuungana na mume wake,  Walipokua wakiongea mama Peter alibaki na mumewe, alimwambia mumewe unadhani Peter kuwepo hapa ndiyo utapona, wewe huponi leo mbona",

baba Peter alimuangalia tu mkewe na kutikisa kichwa. Peter aliagana na wazee wale kisha akarudi alipokua baba yake, hakusema neno lolote zaidi alimnyanyua baba yake na kwenda naye chumbani kwake na kusubiri kesho itakuaje.

alimtaarifu Pricila kwa kumtumia ujumbe wa maneno kwani hakutaka kuongea kuhofia mama yake kulitambua hilo. pricila alimtakia kila jema mume wake.

Asubuhi ilipofika Peter alimuaga baba yake nakusema hatochelewa kurudi huko alikokwenda, baba alitikisa kichwa tu, Peter alimfuta jasho baba yake nakutoka bila kumuaga mtu yeyote,

walikutana walipohaidiana mzee Ayoub na kisha safari ilianza, walifanikiwa kufika walikaribishwa na kijana akawapeleka ndani,

aliwakaribisha ndani kisha mzee Ayoub alianza kwa kujitambulisha na baadae Peter alifuata. Yule kijana mganga alilitambua kama Ally alisema poleni sana na matatizo ya huko mtokako,

kisha alisema mimi si muongeaji sana mtaona ninyi wenyewe mambo yalivyo, Peter na mzee Ayoub walitazamana kisha Ally akachukua kidishi kilichokua na maji,

alichukua dawa kama ungaunga alinyunyuza kisha alisema maneno ambayo aliyaelewa yeye tu kisha aliwaambia tazameni,

maskini Peter na mzee Ayoub waliona kila kitu kilichotendeka zaidi Peter alilia baada ya kimuona mwanae akifanya mambo yale makubwa na ya ajabu, MAMA NAKUCHUKIA,

ITAENDELEA............. SEHEM YA 9
Imeandikwa na kutungwa
                                      NA AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here