mwanangu mimi huyo naishi nae chumba kimoja na ninalala naye kitanda kimoja lakini nimekua mvumilivu ndiyo maana nimeamua nikuambie ili ukisikia nimekufa ujue ni mke wangu ameniua maana baada ya hiki hatoniacha mzima kabisa, je Peter atafanya nini?
SASA ENDELEA................
aliposema maneno hayo alilia sana huku akisema "NAMCHUKIA MAMA YANGU,
namchukia sana, baba alimbembeleza mwanae huku akisema usilie mwanangu na wala usimchikie mama yako ila tujue tunafanya nini sasa ili kuokoa maisha yetu na pia yakwake aachane na hali hiyo,
Peter aliendelea lia huku akisema mchawi ni mchawi baba tena nimebadilisha mawazo naondoka na mke wangu turudi nyumbani nikamchukue.
Kumbuka nyumbani siku hiyo alikua hajisikii vizuri, basi mama yeye alikua busy na kazi zake za hapa na pale mara alisikia sauti mtu akilia,
alikimbia kwenda chumbani alimkuta Pricila ameketi chini akilia kwa uchungu huku akijipigapiga mapajani mama alichanganyikiwa alitoka nje ili apate msaada,
baadhi ya majirani waliokua majumbani walifika pale, mama Peter alipokua anahangaika kumpigia simu mwanae aliona gari la Peter linarudi,
hakushangaa kwani kwa wakati huo alikua anawaza Pricila tu, Peter alipoona nyumbani si pakawaida aliongeza mwendo, alifika nyumbani,
lakini kilichomshtua mama kwenye gari walishuka watu wawili tena wakionekana hawapo sawa, kwani macho yao yalionekana yametoka katika kilio kizito,
lakini Peter na baba hawakujal Peter aliingia ndani alimkuta mkewe na hali mbaya hivyo alisaidiana na baadhi ya akina mama kumuweka vizuri kisha kumuharakisha katika kituo cha afya kilichopo karibu kwani alikua na hali si nzuri,
walipokelewa vizuri wakafuata utaratibu na kisha Pricila alipelekwa chumba cha akina mama wenye hali kama ya kwake.
Huku nje Peter hakua na raha hata kidogo na kwa muda huo mama ndiye aliyekua na mambo mengi yakufanya kuhusu mgonjwa hivyo Peter walikaa nje na baba yake,
baba alisema mwanangu kama Pricila akijifungua tafadhali sana kesho tukiruhusiwa tu msifike kabisa nyumbani sijui utafanyaje ila jitahidi kufanya hivyo,
kisha mama alitoka akasema mwanangu Peter, Peter aliinua uso wake lakini alishindwa zuia machozi yaliyokua yakitoka, usilie mwanangu, mwenzio atakua sawa kinachotakiwa muombee Mungu ajifungue salama".
Alivyosikia maneno yale kutoka kwa mama yake Peter akasema "
kweli shetani amejiinua hana hata aibu kusema Mungu akati usiku anakula watu, eeh MUNGU usituchoke sisi ndo viumbe wako,
mama Peter nae akajisemea yaani huyu mwanaume ngoja wanangu waondoke atanitambua, basi asubuhi wakaondoka walifika nyumbani kuandaa chakula cha mchana kwa ajili ya mgonjwa. Siku hiyo iliisha hivyo yaani kwenda na kurudi hospitali,
mpaka siku ikaisha na Pricila alikua bado zaidi ya uchungu tu, walirudi nyumbani, Peter hakulala alikua anawaza mkewe tu,
alijaribu kupiga simu ya mkewe ilikua ikiita tu bila kupokelewa. Usiku hali ya Pricila haikua nzuri nesi alimuita daktari, basi daktari alitambua Pricila anakaribia jifungua hivyo alianza muhudumia mpaka alipojifingua salama,
Pricila alipomaliza kwakwel hakua na nguvu tena hivyo alilala usingizi mzito mpaka asubuhi, asubuhi aliamka daktari alimpa hongera kwani alikua amejifungua mtoto wa kiume,
alipokua akipokea taarifa hizo familia yake ilikua inaingia basi wote walifurahia taarifa hiyo kutoka kwa daktari, Peter alifurahi alimkumbatia mkewe,
mama alimchukua mtoto akawa anajisemesha "baba Peter mimi ndiyo nimepata mume hivyo wewe sikutaki tena"
Pricila alicheka kwani mpaka kipindi hicho hakujua chochote kinachoendelea hivyo ilibidi wote wacheke,
Pricila akala chakula alicholetewa kisha waliruhusiwa kuondoka lakini Peter akasema mama mimi siunajua nilikua na siku mbili leo ya tatu acha turudi maana Pricila pia atatakiwa aende hospitali kubwa kwa uangalizi mzuri,
mama akasema mwanangu haiwezekani itabidi mjukuu afike nyumbani kwanza mtaondoka kesho basi alafu na sisi tutafuata mbona hiyo haina shida yoyote, Pricila maskini pia aliungana na wazo la mama kwani hakujua lolote,
walitazamana kisha walikubali japo kishingo upande. Walifika nyumbani, palikua pamechangamka kumbe mama Peter aliita rafiki zake kusherekea ujukuu, kwa Pricila
ilikua raha tu kwani hakujua chochote basi alikua akifurahi tu, wale wageni walikua wakimshika mtoto na wakimsifia basi Peter na Pricila waliingia ndani,
mama Peter alibaki nje na ndugu zake watafurahia ujio wa kichanga, huku wakiandaa chakula cha mama kichanga kwani mtoto huyo hakupewa jina kwanza. Basi aliandaa chakula kizuri kwa mkwe wake,
rafiki zake walipomaliza kazi zao pale waliaga na kuondoka na kuacha familia ikiwa na furaha. Muda hauchelewi ndugu msomaji masaa yalikua yanakimbia usiku ukafika walikula kisha waliaga kwenda kulala kwani kwa sasa walikua wakishinda na Pricila chumbani,
usiku ulipofika mama Peter hakukubali upite hivihivi alidhamiria kupandikiza kitu kwa mjukuu wake basi ili asionwe na yeyote alipuliza dawa yakufanya nyumba nzima walale kisha aliingia chumbani kwa watoto wake
akamchukua mtoto nakumchanjia utosini, mtoto alianza kulia mama Peter alirudi kitandani akaigiza kalala kisha alianza ita baba Peter baba Peter, baba peter aliitika kuna nini?sikia mtoto analia, baba Peter akasema ni kweli, basi walitoka wakaone waliwakuta Peter na pricila
wanabembeleza, mama akasema mnyonyeshe, Pricila alipojaribu mnyonyesha mtoto alikataa basi mama Peter alimchukua akaanza muambia vimaneno eeh mjukuu wangu jamani, haya nyamaza mkeo nimekuja nyamaza baba, basi katoto kalitulia tuli kama kalikua hakalii. Pricila
alitabasamu kisha akasema kila mtu na mke wake bwana baba umeshaporwa basi maneno yale yaliwafurahisha, ila baba alisema moyoni ni lazima kesho muondoke maana simuamini mke wangu hata chembe,
maskini baba Peter alikua kachelewa kwani mama mda fupi tu kafanya mambo kweli usilolijua ni sawa na usiku wa kiza kinene.
Basi walirudi kulala na safari hii wote walilala vizuri mpaka asubuhi. Asubuhi waliamka Peter alijiandaa lakini mama alimuandaa Pricila kwani hakua vizuri alipomaliza kumuandaa alianza kumwambia mjukuu wake,
mume wangu ntakuja kukutembelea si unajua nakutegemea Pricila alicheka tu mama nae unavyoongea na mtoto kama anasikia mama alijibu kama utani lakini alimaanisha,
wanasikia kuliko watu wazima hawa"
wakacheka, Peter aliita jamani vipi mbona hamtoki tunachelewa, mama akajibu tayari baba,
ITAENDELEA............. SEHEM YA 6
Imeandikwa na kutungwa
NA AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter
No comments:
Post a Comment