NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 4 - TRUST ME

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, April 16, 2018

NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 4

TULIPO ISHIA.........
Nakweli asubuhi ilikua imefika Peter na mkewe waliamka walishangaa tayari wazazi wameamka baba anafagia na mama anaosha vyombo.
                                    
SASA ENDELEA...............
Basi walisaidiana kazi na baadae wakanywa chai. Peter alitumia muda huo kuaga kwani wote walitakiwa kazini kwahiyo ilimbidi aondoke nakuhaidi kurudi,

 wote walisikitika lakini hawakua na lakufanya. Kipindi Peter anaingia kwa gari ili aondoke baba akasema"Peter mwanangu naomba unibebe mpaka mbele hapo nikamuone rafiki yangu"

haina shida Peter alijibu, mama alichezwa akili alijiwazia moyoni "mmh huyu muongo lazima anataka amuambie kilichotokea na mimi sipo tayari"

akaropoka baba Peter kwanini usiende baadae kuna kitu nataka tuongee hapa, baba Peter hakukubali akasema lazima nimuone muda huu, mama akasema sawa basi usichelewe kurudi basi baba alikubali japo kishingo upande. Walipanda gari wakaondoka ila walipofika mbali baba Peter alimuomba Peter asimamishe gari kwani alisema anamaongezi nae,

alipokua anasimamisha gari, baba nae alikua akijiandaa kutoa taarifa aliyodhamiria kutoa, mwanangu baba alianza, lakini alipokua anaanza tu Peter alimuona mama kwa mbali anakuja mbio,

alimpiga baba yake begani akimuonesha alipotokea mama, baba alishangaa kumuona akatikisa kichwa kwa hudhuni sana, basi mama alifika pale anahema ovyo yani kiasi kwamba akashindwa kuongea kisha alijikaza akasema baba Peter kuna mgeni nyumbani anakusubiri,

Peter alishangaa sana, baba Peter alikubali kwani hakutaka Peter asijue kitu. Alishuka kwa gari Peter aliaga akaondoa gari, mama Peter alianza jamani mume wangu si nimeomba msamaha jamani mbona unataka mwambia Peter, unataka anichukie?

baba Peter alitikisa kichwa kisha akasema kweli shetani ameamua kujiinua, huna hata aibu, basi baba Peter alimpisha mkewe na kuondoka. Basi alirudi nyumbani na mkewe pia alifuata, Pricila hakuisi chochote kibaya kwani wale ni wazazi wake na hakuwahi waona wakigombana hivyo aliwapenda sana.

Peter alifika nyumbani akiwa na mawazo sana alifikiria baba anataka mwambia nini, na ile hali iliyotokea pale mama kutokea ghafla na mbn baba hakuwa na amani lazima kuna kitu ntatafuta ruhusa siku mbili hizi nirudi nkajue kuna nini, hiyo ilikua ahadi ya Peter.

 kesho yake Peter alifika kazini nakuanza kazi ya kuomba ruhusu haikuwa kazi ngumu sana kwake kwani bosi alimuamini kutokana na uchapakazi wake lakini

alimsisitiaza kua makini na mke wake kwani anahitaji mtu wa karibu sana kwa sasa. Basi Peter alishukuru na akaondoka, akawaaga wafanyakazi wengine,

wengine walishaanza muita baba kijacho walicheka wenyewe kisha Peter akaondoka, hakurudi tena kwake aliendelea na safari mpaka kwa wazazi wake. Alipofika wote walishangaa walihisi kuna tatizo lakini Peter alitabasamu kuna kitu nilisahau hivyo ntaondoka kesho kutwa,

wote walifurahi wakatabasamu lakini Pricila alijisemea moyoni mmh huyu mwanaume kanikimbuka mara hii hana lolote basi alimkumbatia. Peter alitabasamu akisema moyoni baba ni lazima lazima nijue kuna nini, huku mama Peter akisema nitajitahidi baba Peter alinyanyue mdomo kumueleza Peter,

baba Peter nae alijisemesha moyoni akisema ntatumia akili zangu zote Peter atambue kinachonitesa baba yake, basi kila mtu aliwaza Lake,ndugu msomaji kuanzia siku ile mama Peter alikua karibu na Peter kiasi kwamba baba Peter alikosa mda na mwanae,

alijifanya kumfundisha peter jinsi ya kuishi na mkewe. Baba Peter alipiga mahesabu afanye nini ili amueleze Peter maana kesho ataondoka basi alimfuata Pricila alipokua ameketi, mwanangu naona umechoka mwenyewe 

naelekea kwa rafiki yangu mbele huko ila mwanangu naomba mwambie Peter kesho nina mazungumzo nae hivyo anapoondoka anipitie eneo aliloniacha siku ile, ila tafadhali mwanangu naomba usimwambie mbele ya mama

utamwambia mkiwa ndani chondechonde mwanangu kisha alicheka hahha mwanangu nakuona mwenyewe Pricila nae akajichekesha nakusema "

haina shida baba ntafikisha ujumbe"lakini alijiuliza moyoni Pricila ni mazungumzo gani hayo mama asijue kisha alitabasamu akasema haya baba mambo ya wanaume haya.

 Ilipofika usiku basi Pricila alifikisha ujumbe kwa mume japo mume alionekana kua na mawazo, lakini baada ya ujumbe ule alitabasamu Pricila aligundua hilo akadadisi kuna nini kipenzi?,

Peter alijichekesha nakusema"mke wangu nilikua nawaza hapa ubaba unanijia afu baba naye hanipi hata maneno asa uliponiambia ana mazungumzo na mimi nimefurahi, Pricila akahoji lakini mbona kasema mama asijue,

Peter akasema utawaweza wazee hawa wanapenda ishi kukomoana, basi wakacheka sana kwani ukweli ni kwamba Pricila yeye alipenda kucheka mumewe alijua hilo, ikawa usiku, ikawa asubuhi,

baba Peter aliamka mapema alimuaga mkewe kwamba anawahi shamba akachimbe mihogo kwani anahamu sana na mihogo, mkewe hakubisha hivyo alimruhusu mumewe, kweli aliondoka, mama aliendelea na kazi lakini Peter aliamka, Pricila alibaki ndani, baada ya Peter kimsalimia mama, mama akauliza hali ya Mkwe wake,

Peter hakajibu hajisikii vizuri leo, mama alitabasamu akasema ndiyo siku za mwisho hizi lazima ajisikie vibaya, Peter akamkumbusha mama yake kwamba siku yake yakurudi kazini imefika, mama hakubisha kwani alijua taarifa hiyo,

 Peter alizuga kumuulizia baba yake, mama kwa tabasamu akajibu, baba yako kaamka na hamu ya mihogo kaenda zake shambani, wote walicheka,,

Peter aliingia ndani akajiandaa haraka haraka alimuaga mke wake nakuhaidi kurudi tena kumjulia hali, aliingia katika gari aliendesha mpaka alipofika sehemu ile alimkuta baba yake, baba aliingia ndani ya gari aliomba mwanae asogeze mbele mama asijetokea tena Peter alifanya hivyo.

Baba alianza kwakusema inahitaji ujasiri mwanangu nisikilize vizuri. Baba peter alimuhadithia mwanae kwa uchungu huku akilia, Peter alishindwa vumilia akasema "mama yangu anaroho ya shetani namna hiyo, mama amekua simba mla watu baba,

ni lazima nirudi nikamchukue mke wangu akajifungulie mjini mimi namuogopa mama yangu,
baba alimuonea huruma Peter kisha akasema"

mwanangu mimi huyo naishi nae chumba kimoja na ninalala naye kitanda kimoja lakini nimekua mvumilivu ndiyo maana nimeamua nikuambie ili ukisikia nimekufa ujue ni mke wangu ameniua maana baada ya hiki hatoniacha mzima kabisa, je Peter atafanya nini?

ITAENDELEA............. SEHEM YA 5
Imeandikwa na kutungwa
                                      NA AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here