NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 7 - TRUST ME

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, April 21, 2018

NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 7

TULIPO ISHIA............
mtoto alisimama kisha akasema kuanzia leo ukifika huku utaongea na utatembea basi wote walishangilia, ISAYA alisimama kisha akasema kwa sauti nzito ASANTEEEE,
                     
                                 
 
SASA ENDELEA...........
wote walipiga makofi nakusema sasa tumepata mwenye nguvu, bibi alifurahi sana akasema"jamani furaha ya yangu haielezeki ila leo naombeni mnipe jibu kuhusu nini

nimfanye mume wangu maana naona ananisumbua sana mimi, wote walinyamaza kisha Isaya akasema kazi hiyo niachie mimi bibi nisubiri hapa narudi, kisha alijikung'uta miguu nakupotea yaani kama mtu mzima kumbe mtoto hata mwezi hajamaliza lakini kwa uchawi wa bibi yake yote yaliwezekana.

Hapa natamani niseme kuna watu kwa macho ya kawaida ni vilema lakini katika ulimwengu wakichawi watu hawa wanakua na nguvu zote za miguu au mikono kulingana na watakavyo ili kazi zao ziende sawa,

watoto wadogo kama isaya tayari anabebeshwa mambo magumu sana na anayaweza kupitia nguvu za kichawi. Basi mtoto Yule alifika kwa babu yake aliyekua amelala katika mkeka alimgeuza kisha alimkalia usoni alipomaliza alikua kamyea usoni kisha alitumia mkono wake kumlisha kinyesi kile, baba Peter yeye alikua kama mtu anayeota,

kwani alikua akijigeuza geuza, Isaya alipomaliza alicheka Sana kisha aliyeyuka na kurudi porini wote walifurahi kumuona karudi bibi akasema kweli vyakurithi vinazidi sasa nitakua nina raha tu,

tuambie umemfanya nini, Isaya alicheka kisha akasema nimemlisha kinyesi changu na kitamsumbua sana kwani nimekinuia hivyo na watu watatafuta tiba lakini hawezi kupona Yule hahahhahahhahahah,

alicheka kwa nguvu wote walifurahi kisha mama Peter alimrudisha Peter katika hali yake ya kawaida na kikao kilifungwa kisha alimrudisha nyumbani, aliona wanae wakisikitika kisha akasema"

asanteni kwakuniletea mwanaume"alimlaza kisha aliyeyuka. Peter alishuhudia mtoto alipokua akijinyoosha alianza kuangaza huku na kule Pricila akamuuliza mumewe kuna nini?

 Peter alishindwa mjibu mke wake lakini Pricila naye akili yake yote ilikua kwa mwanaye hivyo alimchukua akamnyonyesha kisha mwanaye akalala tena,

 tulale mume wangu, Peter hakua mkaidi kwani moyo wake tayari uliongeza chuki kwa mama yake mzazi kutoka na tabia chafu alizonazo.

Walilala usingizi na kesho yake walichelewa kuamka kwani usiku walikesha wakisuburi mtoto aamke. Kwa wazazi wa Peter mambo hayakua mazuri hata kidogo kwani baba Peter alikua ameamuka vibaya sana, alikua akiharisha sana, mwili unavuja jasho kama kamwagiwa maji,

na kla alipojaribu kuongea alitapika vibaya mno. Hali hii kwa mama Peter ilikua burudani hivyo alifanya kazi zake, alipomaliza alimpigia Pricila akasema"habari za kwenu mwanangu,

leo nimewakumbuka haswa mjukuu wangu, weka simu masikioni mwake nimsalimie"maskini Pricila hakujua kitu chochote alicheka kisha naye alisema"mama na mjukuu wako kama atakusikia vile haya msalimie",

mama Peter alianza mwambia Isaya wewe ni balaa yani huku hapakaliki mengine tutaongea kilingeni, kipindi anaongea huko Isaya alikua anacheka nakutabasamu tu, Pricila alifurahi tu akachukua simu akasema"

yaani mama ukimuona huyo mjukuu wako alivyofurahi sasa kama anakuelewa, mama Peter alijichekesha na kusema malaika wadogo hao wanauwezo mkubwa kutushinda sisi watu wazima mwanangu kisha alibinua midomo, haya mama asante sana fanya uje basi,

sawa mwanangu nitakuja tu, waliagana na simu ilikatwa. Baba Peter siku nzima ulikua ni mwendo wakuharisha, kuvuja jasho na kutapika yaani ndani ya siku moja alikua hatamaniki.

Na mkewe aliketi nje tu akiendelea kusuka mkeka wake. Baba Peter alipokua akienda chooni alijigonga akaanguka, mke wake akasema wewe bwana tusianze kusumbuana kuharisha tu unajidekesha hivyo,

baba Peter alimtazama mke wake kisha chozi lilimtoka. Mama Peter alijua kamkosea mumewe akajisemea moyoni, hapa lazima niwe mpole asijejua kama mimi nahusika,

jamani mume wangu pole utakua sawa tu, ngoja nikupeleke ndani, nikuletee chakula alafu ukaoge. Baba Peter hakua na neno kwani kwa wakati ule hakuna alichoweza kufanya zaidi yakulia tu.

 Basi mama Peter alimuandalia mumewe chakula akamiwekea chini alipokua amekaa kisha akasema jitahidi ule mimi nikakuchulie maji uoge maana hilo limeanza kutoa harufu, hakujali kwamba mume wake anahitaji kulishwa kwa wakati ule.

Mama Peter alitoka nje akachukua ndoo yake nakuanza safari, alipokua njiani alikutana na rafiki yake, walianza msifia Isaya nakusema yule mtoto moto wakuotea mbali maana huko nyumbani hapakaliki,

walipiga umbea wa hivi na vile walipomaliza waliagana. Lakini jirani na kwa wazazi wa Peter palikua na mzee mmoja na mkewe mzee huyo aliitwa mzee Ayubu,

walishirikiana mambo mengi na baba Peter lakini baba Peter hakuwahi mwambia kuhusu mkewe japo maneno hayo yalisikika kijiji kizima.

Mzee Ayubu alisema mke wangu, mbona hii si kawaida ya baba Peter mpaka inaelekea jioni hatujaonana, mama Ayubu ambaye ni mkewe akasema ni kweli mume wangu nilidhani mmewasiliana,

hapana mke wangu ngoja nikamuone, alisema mzee Yule nakuanza safari ya kwenda kumuona rafiki yake. Alipofika nyumbani palikua pametulia sana lakini mlango ulikua wazi, alisogea nakuanza kuita, alipokua akiendelea kuita

alishangaa kumuona baba Peter anatoka kwa kutembelea magoti maskini Ayubu alisema "baba Peter kuna nini tena?, kisha alimsogelea hakuamini kuona jasho lile likitiririka mwilini kama kuna mtu anamwagia maji,

alimshika vizuri ili kumuuliza baba Peter alipojaribu kuongea alitapika sana alipomaliza alikaa chini nakuanza kulia kuashiria kachoka hawezi kitu anahitaj msaada.

 Ayubu roho ilimuuma machozi yalimdondoka tu alipoangalia pembeni aliona chakula lakini hakijaguswa alipojaribu mlisha baba Peter pia alishindwa na kutapika

ITAENDELEA............. SEHEM YA 8
Imeandikwa na kutungwa
                                      NA AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter                             

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here