NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 2 - TRUST ME

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, April 14, 2018

NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 2

TULIPO ISHIA........ 
   . Walienda sokoni walifanya manunuzi ya muhimu bila kasahau vyakula kwani Peter hakutaka mke wake akapate shida ya vyakula. Walimaliza manunuzi hayo kisha walirudi nyumbani wakisuburi siku inayofuata waende kijijjni.
                        
 SASA ENDELEA......
 Kijijini kwa wazazi wa Peter maisha hayakua magumu kwao kwani Peter aliwahudumia vizuri wazazi wake kwani yeye alikua mtoto wa pekee. Hawakua na shida ya kitu chochote pia wazazi hawakua wazee kiasi eti washindwe kufanya shughuli za kilimo hivyo pia walijishughulisha na kilimo.
Japo walikua na maisha magumu lakini baba Peter alikua na jambo lililomsumbua sana akili yake mda mwingi alikua akikaa pekeyake nakujiinamia ndipo siku moja aliamua kumuita mke wake ili wazungumze akihisi atakua sawa kiakili,
 "mama Peter, njoo mke wangu", baba Peter alimuita mkewe kwa upendo kabisa, kunani tena mume wangu?sawa nakuja sasa hivi, aliitikia mama Peter. Baada ya dakika chache alifika pale alipoitwa.
 "mke wangu kuna maneno nayasikia tu na yananichanganya na nimeishi na wewe muda mrefu sasa sijawahi kuona na mambo ninayoyasikia, hivi mke wangu kweli wewe ni mchawi"?

, alipofika hapo mama Peter alishtuka kisha alirudia lile neno mchawi!!!! Ndiyo baba Peter wala hakusita aliendelea ndiyo mke wangu ndio maana leo nimekuita ili tujue tutafanyaje, alimaliza. Mama Peter aiinamisha kichwa chini kuonesha kuchanganyikiwa na swali lile kisha akasema "mume wangu ndivyo walivyo binadamu

wanatuonea wivu tu hawana lolote hao kisa mume wangu unanipenda hatuna shida basi wanataka kutogombanisha kisha alijichekesha tehtehteh!!!! Baba Peter alitabasamu kuonesha kaelewa lakini alihisi kitu pale kisha akasema nimekuelewa mke wangu kaendelee na kazi zako

 yaani binadamu buana wabaya sana baba Peter alijisemesha, kisha mke akajibu sana akambusu mume wake shavuni kisha akaondoka kuelekea ndani. Baba Peter aliamua kumfuata ndani lakini alipofika tu mlangoni alisikia mke wake akijisemesha "

afu hili nguruwe naona limeanza kunifuatilia tena likiendelea nitalipoteza mimi au hanijui vizuri eti nimesikia ata angeona angejijua mwenyewe na bado,

baba Peter alikohoa, mke wake akashtuka kisha akajikaza kisabuni akatoka alipofika mlangoni alimsukuma mumewe kisha akasema hivyo ulivyosikia ndivyo ilivyo sasa utajijua wewe kisha akaendelea na mambo yake baba Peter Alibaki ameduwaa akarudi katika kiti alijiinamia akionekana mtu mwenye mawazo sana. Alipokua katika hali hiyo

alishtushwa na muungurumo wa gari alipoangalia alikua ni mwanae Peter basi alifurahi sana akaanza kuwakimbilia walipo.

 Alifika akawakumbatia wanawe nakuanza wapokea mizigo huku akimlaumu Peter kwanini hakusema mpaka mimba ya Pricila inakua kubwa hivyo. Peter aliomba msamaha nakusema

 "baba yangu kazi nyingi sana lakini ndiyo sababu leo tupo hapa uone kwa macho yako"basi baba akasema haina shida mwanangu karibuni sana.

  Baba Peter akasema "msijali wanangu karibuni sana nyumbani"baba alisema hayo huku akimshika mkono Pricila, Pricila alikua binti mzuri sana kisura mpaka tabia zake hivyo wazazi hawakua na kinyongo na binti.

 baba Peter aliingiza mizigo ndani kisha alitoka na jamvi kubwa alitandika chini kisha wote waliketi chini. Walikua na furaha sana yaani utani wa hivi na vile baba Peter akimsifia mwanae kwakua kaonesha yeye ni kidume huku mzee akisema mwanangu unajua kuchagua sijui ulimtoa wapi binti huyu,

 wotee walicheka kisha Pricila akauliza baba, kwani mama yuko wapi?hahahhaha baba Peter hakujua umeona Peter yaani mwanangu yeye na mama yake tu mie walaa hanipendi hata, hahhahahah aliongea hayo kwa utani mara wote walicheka, walipokua wakicheka wakasikia sauti

"jamani wanangu hao", alikua ni mama akiwa na ndoo kichwan ilionesha ametoka kisimani kuteka maji basi aliitua ile ndoo kichwani wanae wakainuka nakumkumbatia mama yao.

Jamani mbona ghafla hivi hata hamsemi, Peter na Pricila walitazamana kisha wakatabasamu, kisha mama akasema tena mmmh mwanangu mpaka tumbo linakua hivi hata usemi nije kukusaidia kazi nyumbani jamani tunaugomvi?

ITAENDELEA............. SEHEM YA 3
Imeandikwa na kutungwa
                                       A AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter                                            


USISAHAU KUACHA MAONI YAKO KWA KUCOMMENT APO CHINI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here