NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 1 - TRUST ME

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, April 13, 2018

NAMCHUKIA MAMA YANGU SEHEM YA 1


 NAMCHUKIA MAMA  YANGU SEHEM YA 1 IMEANDIKWA NA  AGATH FRANCIS    
                                                  

 Pricila na Peter ni mke na mume walioishi maisha ya furaha sana. Japo makwazo yapo lakini waliyahimili kwao hawakuruhusu ugomvi. Pricila alimuheshimu sana peter wake kwani huyo ndiye aliyekua kila kitu kwake hakua na ndugu mwingine wa karibu sababu wazazi wake walifariki pindi alipokua mdogo,

 hivyo basi wazazi wa peter aliwafanya wazazi wake na Peter kua kila kitu kwake. Siku kadhaa zilipita katika ndoa yao wakidumisha furaha hiyo lakini kuna kipindi Pricila hakujisikia vizuri hivyo aliona sio vibaya akimshirikisha mumewe. Basi ilikua jioni tulivo Peter alikua katoka katika mihangaiko yake ya kila siku,

 Pricila aliandaa chakula mezani wakala kama kawaida yao walikua wakilishana huku wanacheka kwa furaha kisha Pricila akasema baby nikuambie kitu, mmmh Peter aliguna kisha akasema kitu gani hicho, haya niambie wife wangu!!, "baby mwenzio siku hizi ata sijisikii vizuri nahisi ninaumwa yaani nipo ovyo sana naomba nisindikize hospitali baba yangu

"Pricila alimaliza, usijali mke wangu itakua unahoma hivyo basi kesho mapema ntaomba ruhusa mapema nikusindikize sawa mama yangu, basi Pricila kwa madeko alitikis kichwa kuonesha kukubali. Kesho ilifika asubuhi Peter alijiandaa kuelekea ofisini na mke wake alikua bado kajilaza kitandani kisha Peter akamkumbusha mke wake ajiandae maana atarudi mapema kumchukua ili waende hospitali

Basi waliagana Pricila aliinuka akafanya kazi zake japo kwakujivuta kisha alianza kujiandaa na alipokua akimalizia kujiandaa mumewe aliingia ndani kisha akasema "cha madeko wangu bado tu"alimaliza, hahahhahah!!!pricila alicheka kisha akajibu tayari buaaana. Basi walimaliza wakaingia katika gari yao ndogo safari yakuelekea hospitali ikaanza.

 walipofika hospitalini walimuona daktari, kisha daktari alichukua maelezo ya Pricila kulingana na alivojieleza, akawaandikia vipimo na kuwaelekeza maabara sehemu ambayo vipimo hufanyika.
Waliingia maabara mtaalamu wa maabara aliwachukua vipimo nakuwaomba wakae nje wakisuburi majibu. Baada ya dakika kazaa majibu yalikua tayari hivyo walipewa karatasi ile ya vipimo kisha waliombwa kurudi kwa daktari.

Daktari alianza kwakusema "jamani hongereni sana niliandika vipo kadhaa hapa lakini majibu yanaonesha una ujauzito wa miezi mwili",

alipofika hapo alitulia kidogo kisha Pricila na Peter walitazamana kisha wakacheka, daktari aliona furaha ya wawili hao aliwapa hongera na kumsisitiza kufuata yote muhimu aliyomuelekeza ili kua na afya njema.

Waliingia ndani ya gari wakiwa na furaha yaani njia nzima vicheko wakitaniana mtoto wakike mara wakiume basi burudani, sio kama akina fulani mke akipata mimba basi sura kama kanywa juice ya limao basi walifika nyumbani wakiwa na furaha zao.

 Maisha yaliendelea kua mazuri kwa wawili hao hakuna chochote kilichoharibika kwao, upendo uliongezeka mara dufu, Peter alimuhudumia mke vizuri kabisa na tumbo nalo lilianza kujichomoza mbele kuonesha linafurahia matunzo ya wawili hao,
walisindikizana clinic kujua hali ya tumbo hilo maramara, manesi na baadhi ya madaktari waliwapongeza kwa namna wanavopendana.

wapenzi wasomaji kama mjuavyo siku hazigandi na hatimae miezi ilisogea mbele ndipo Peter alipo amua kumueleza hili mke wake, "mke wangu unaonaje tufanye maandalizi yote muhimu alafu nikupeleke kijijjni ili ukapate ukaribu wa wazazi maana mimi nakua kazini, ila ukiwa kwa wazazi watakupa ukaribu wa kutosha, unalionaje hili mke wangu?

Ooooh wazo zuri sana mume wangu yaani mimi nakusikiliza wewe baba yangu isitoshe hatujawaona wazazi kitambo sana bila shaka wao pia watafurahia uwepo wetu, alijibu Pricila akionesha sura iliyochangamka sana

akiashiria kuunga mkono wazo la mume wake Peter. Basi Peter nae alilitambua hilo kisha akasema ndiyo maana nakupenda malkia wangu unanisikiliza sana na kuheshimu mawazo ya mimi mumeo.

Hapa naomba niseme kidogo watoto wakike jamani wanaume wanapenda kusikilizwa na kuheshimiwa mawazo yao kwahiyo basi muunge mkono mumeo kwa zuri akuambialo na kama unapinga basi mjibu kwa sababu akuelekewe tena kwa utaratibu sio kupayuka kama tufanyavyo,

walimaliza mazungumzo yao kwa amani kabisa na kukubaliana kesho yake wataanza maandalizi kama walivyopanga kwani muda wa Pricila kujifungua ulikaribia. Basi kesho yake walifanya ya muhimu na kwakuwa ilikua mwishoni mwa wiki Peter hakwenda kazini alitumia muda wake na mkewe. Walienda sokoni walifanya manunuzi ya muhimu bila kasahau vyakula kwani Peter hakutaka mke wake akapate shida ya vyakula. Walimaliza manunuzi hayo kisha walirudi nyumbani wakisuburi siku inayofuata waende kijijjni.
                 ITAENDELEA............. SEHEM YA 2
Imeandikwa na kutungwa
                                       A AGATHA FRANCIS
instergram francisagathathestorywriter 

Tupe maoni yako kwa kucomment apo chini

1 comment:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here