JESHI la Polisi mkoani Dodoma, baada ya kumkamata na kumfanyia
mahojiano Onesmo Machija (44) anayejiita ‘nabii’ Tito, kutokana na
mahubiri ya kidini anayoyafanya, limesema mtu huyo ana matatizo ya
akili.
Akizungumza na wanahabari mjini Dodoma leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Dodoma, Gillesi Muroto, amesema mnamo Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi
kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili
chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la William ambapo
aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo
lakini hakurejea.
Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba baada ya hapo, Machija ambaye
kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika
kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom)
akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya
kidini.
Kwa msingi huo, alisema jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa
ya Mirembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo
hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dkt. Dixon Philipo
aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo.
Pamoja na hayo, Muroto alisema jeshi la polisi mkoani humo bado
linaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili
kufanya uchunguzi zaidi.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment