GARI la kwanza lililotengenezwa Rwanda, linatarajiwa kuwa barabarani
Mei mwaka huu, imefahamika. Kampuni ya kutengeneza magari ya Volkswagen
(VW) ya Ujerumani, ipo kwenye maandalizi ya kutengeneza aina tatu za
magari nchini humo.
VW imetangaza kuwekeza Dola za Marekani milioni 20 (takribani Faranga
bilioni 17 za Rwanda) kwenye uanzishaji kiwanda cha kutengeneza magari
nchini humo. Uongozi wa kampuni hiyo umesema sehemu kubwa ya fedha hizo,
zitatumika kutengeneza magari na kuanzisha maeneo ya uunganishaji
magari.
Kampuni hiyo tayari imesajili kampuni nchini humo iitwayo, Volkswagen
Mobility Solutions Rwanda. Wakili Athanase Rutabingwa ni Mkurugenzi
Mkazi wa kampuni hiyo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa VW nchini Afrika Kusini,
Thomas Schafer alisema, wamechagua kuwekeza Rwanda kwa kuwa kuna
mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Schafer pia ni mwakilishi wa VW barani Afrika. “Tulichagua Rwanda kwa
sababu kuna utulivu wa kisiasa, wanapambana na rushwa, ukuaji asilimia
saba (uchumi), idadi ya watu vijana na yenye ufahamu wa teknolojia.
VW inapata msaada mkubwa kutoka Serikali ya Rwanda na ushirikiano
kutoka Bodi ya Maendeleo Rwanda unaongoza ajenda ya Smart City,” alisema
Schaefer. Kutengenezwa magari Rwanda ni matokeo ya kusainiwa kwa hati
ya makubaliano kati ya Serikali ya nchi hiyo na Volkswagen Desemba mwaka
2016.
Pande hizo mbili zilifanya upembuzi yakinifu Septemba mwaka jana na
kuridhika kuwa uwekezaji huo utakuwa na manufaa. “Kenya tunatengeneza
Polo Viva na hapa tunatengeneza aina tofauti. Hata kama tunaanzisha kitu
fulani kipya Kenya, kitakuwa tofauti na kinachotengenezwa Rwanda,”
amesema Schaefer.
Kiwanda cha Rwanda kinatarajiwa kujengwa kwenye eneo la Ukanda
Maalumu wa Kiuchumi (SEZ) na kitakuwa na uwezo wa kutengeneza magari
5,000 kwa mwaka. Kwenye eneo la hilo, pia kutakuwa na duka la kuuza
magari na eneo la matengenezo.
Kwenye awamu ya kwanza, kiwanda cha Rwanda kinatarajiwa kuajiri watu
kati ya 500 hadi 1,000. Schafer alisema kiwanda hicho kinaweza kuanza
kazi kabla ya mwisho wa Mei mwaka huu.
“Tunajaribu kuondoa huu mtazamo kwamba, Afrika ni masikini; hawawezi
kumudu kununua magari,” alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Kigali. Kwa kuanzia kiwanda cha Rwanda kitatengeneza magari
madogo ya kutembelea aina ya Volkswagen Passat, Volkwagen Polo na
Volkswagen Teramont.
VW itatengeneza magari nchini humo kwa kuzingatia mtazamo uitwao
‘ThinkBlue cars’. Mtazamo huo unahusu magari rahisi kuyahudumia, na
rafiki wa mazingira kwa kuwa yanatumia mafuta kidogo na kutoa moshi
kidogo.
Schafer alisema awamu ya kwanza ya VW kwenye uchumi wa Rwanda kwa
kiasi kikubwa, itahusisha ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari na
mafunzo. Uwekezaji wa VW Rwanda utafanywa kwa awamu tatu.
Kwa mujibu wa Schafer, baadhi ya mitambo itakayotumika kwenye kiwanda
hicho ipo njiani kupelekwa bandari ya Mombasa na kwamba kazi zitaanza
haraka kadri itakavyowezekana.
VW wanasema wamevutiwa na ukuaji wa soko la Rwanda na wana malengo ya
muda mrefu kuwekeza nchini humo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya
Maendeleo Rwanda (RDB), Clare Akamanzi, ameikaribisha VW kwenye soko la
Rwanda na anaamini uwekezaji huo utawanufaisha vijana nchini humo.
“Tumefurahi kufungua huu ukurasa mpya kama nchi. Tangazo hili ni
ushahidi wa maendeleo yaliyopatikana tangu tuliposaini MOU mwaka
2016.Tuna uhakika kwamba, ushirikiano na VW utatengeneza fursa nyingi
kwa Wanyarwanda vijana,” alisema Akamanzi kwenye mkutano huo na
waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa Akamanzi, mwaka jana kulikuwa na magari 300,000 kwenye
nchi hiyo yenye watu milioni 12. Amesema, uwekezaji wa Volkswagen nchini
humo ni nyongeza katika ongezeko la uwekezaji kutoka nje ya nchi hiyo.
“Katika miaka 10 iliyopita, uwekezaji ulioandikishwa Rwanda
umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 100 kutoka Dola za Marekani milioni
800 mwaka 2007 hadi Dola bilioni 1.675 za Marekani mwaka 2017.
Huu ni uthibitisho kwamba Rwanda inaonekana eneo lenye mvuto kwa
uwekezaji” alisema Akamanzi. MAGARI YA TANZANIA Wakati hayo yakiendelea
nchini Rwanda, Tanzania nayo inazidi kufanya vizuri kwenye ubunifu na
sasa inatengeneza na kuuza nje magari ya kubeba watalii na malori ya
takataka.
Kampuni ya Hanspaul Automechs Limited (HAL) iliyopo kwenye eneo la
viwanda Njiro jijini Arusha, inatengeneza magari makubwa ya kubeba
watalii maarufu kwa jina la ‘War Bus’. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
kampuni hiyo, Satbir Hanspaul, magari hayo yanauzwa Kenya, Afrika
Kusini, na nchi za Ulaya.
HAL imesema, imebuni na kutengeneza magari ‘spesho’ ya kubeba
takataka yanayofaa kwa mazingira ya Tanzania ikiwemo hali ya hewa, aina
ya barabara na mfumo wa maisha wa wananchi hivyo yatadumu kwa muda
mrefu.
“Lakini aina mpya ya malori ya kubeba takataka si kwa ajili ya
kampuni yetu au kiwanda chetu tu, kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na
TBS (Shirika la Viwango Tanzania), wazalishaji wengine wanaweza
kuyatengeneza lakini kwa kutumia utambulisho wa ubunifu wa HAL kama
kielelezo,” alisema Hanspaul.
Alisema, magari ya kubeba takataka na yale ya watalii ni ubunifu wa
Tanzania unaozivutia nchi nyingine zikiwemo za Ulaya, na kwamba magari
ya watalii yanakubalika kwenye soko la kimataifa.
Magari hayo yenye nembo za Toyota, Nissan na Land Rover
yanatengenezwa kwa kutumia mashine za kisasa zikiwemo robot kama ilivyo
kwenye viwanda vya magari katika nchi zilizoendelea.
HAL ilianzishwa mwaka 2007. MAGARI YA KENYA Viwanda vya kutengeneza
magari havitakuwa Tanzani na Rwanda tu, kwa kuwa kampuni ya VW tayari
ina kiwanda Thika nchini Kenya.
VW ilianza kutengeneza magari Kenya mwaka 2016. Mwaka mmoja baadaye
VW ilikuwa imeuza magari 104 nchini humo. Mwaka jana, kampuni ya
kutengeneza magari ya Peugeot ya Ufaransa ilianza kutengeneza vyombo
hivyo vya usafiri nchini Kenya.
Kampuni ya Toyota ya Japan pia ina kiwanda cha magari nchini humo
kilichoanzishwa mwaka 2015. VW wanapanga kuongeza uzalishaji mara mbili
katika kiwanda cha Thika sanjari na kutengeneza aina mpya ya gari.
Hivi karibuni, Mkuu wa VW Afrika Kusini na operesheni za kampuni hiyo
Afrika, Schaefer alimweleza Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini East
London, nchini Afrika Kusini kuwa wapo kwenye mchakato wa kutengeneza
aina ya pili ya ga
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment