Jarida la Forbes Jumatano hii limetoa orodha mpya ya wanawake 100
wenye nguvu ya ushawishi zaidi duniani (100 Most Powerful Women ) mwaka
2017 kwenye Michezo, Sanaa, Teknolojia, Media na Siasa wametajwa,
ambapo orodha hiyo imeongozwa na Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel.
Wa pili kwenye orodha hiyo ni Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa
May, wa tatu ni mke wa tajiri namba moja duniani Bill Gates, Bi. Belinda
Gates, Tazama orodha kamili ya majina 100 HAPA.
Kwa upande wa majina ya wanawake waliofanya vizuri kwenye kipengele
cha Burudani na Vyombo vya Habari (Media), Mwanamama Oprah Winfrey
ameongoza orodha hiyo kwa mwaka 2017, huku akiwa nafasi ya 21 kwenye
orodha nzima ya majina yote ya kwenye vipengele mchanganyiko.
Mwanamuziki Beyonce ameshika nafasi ya 5 kwenye orodha ya Wanawake
wenye nguvu ya ushawishi zaidi duniani kwenye kipengele cha
‘Entertainment & Media’ huku akishika nafasi ya 50 kwenye orodha
nzima ya wanawake wenye ushawishi zaidi duniani.
Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani mwaka 2016, Bi. Hillary
Clinton ameporomoka kutoka nafasi ya 63 mwaka jana 2016 hadi nafasi ya
65 mwaka huu hii ni baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.
No comments:
Post a Comment